Harmonize Amsifia Diamond Platinumz.



By:Peace Benshazy

Picha:Harmonize na Diamond.

      Harmonize aliposti ujumbe wa kumsifia Ex-Boss wake Diamond kwa kumtoa mbali na kufanya awe alipo sasa hivi.
"Pekee uliona dhahabu kwenye mchanga na giza jingi sanaa.. Leo Hii Africa mzima special East Africa wanajivunia uwepo wangu 🤞♥️This is love is forever my brother. Everything I have done its just to make you proud don't get me wrong kaa chini peke yako bila mtu yeyote pembeni soma ninachomaanisha. You are the legend one. Stay cool#KONDEBOY and all KONDEGANG team we love you. Happy new year big brother",Harmonize ambaye sasa hivi anamiliki lebo ya KONDE GANG alipost ujumbe huo kwenye page yake.
      Siku kadhaa zilizopita Harmonize alimkashifu Diamond kwa kukataa kumsaidia babake mzazi. Hii ni baada ya picha ya babake diamond akiabiri matatu,huku kabeba gunia kusambaa mitandaoni. Diamond na babake hawajakuwa kwenye uhusiano mzuri wa baba na mwana kwa sababu hakumpa malezi akiwa mchanga.

     Katika wimbo wake mpya 'WAPO',Harmonize anasuggest kuwa wazazi wote wanapaswa kupewa heshima. "mama na baba ndio nguzo la maisha,wapende wote,sio wa kike anacheka na wa kiume analia kila saa,"Harmonize anaonekana kutoa wasia huu kwa Diamond.
     Licha ya haya yote,Harmonize bado anamheshimu Diamond na kusema kuwa Diamond ni King. Swali ni je,ujumbe huo wa Harmonize na wimbo wake wa WAPO utachukuliwa vipi na Diamond?

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

How To Start a Music Production Studio

NAIROBIANS FLOODS BUS TERMINUS TO TRAVEL TO UPCOUNTRY IN FEAR OF LOCKDOWN THIS FESTIVE SEASON